Mbunge wa rongai Raymond Moi amesema kwamba ofisi yake imejikakamua kukabiiana na ukosefu wa elimu miongoni mwa kizazi kijacho, kwa kuwekeza katika miradi inayosaidia utendakazi wa sekta hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Raymond alihuzunika kwamba shule nyingi za eneo bunge lake hazina madarasa ya kutosha, huku idadi ya wanafunzi ikizidi vifaa vilivyoko.

“Katika bajeti ya mwaka wa kifedha 2015/16, CDF ya Rongai imetenga fedha za ujenzi wa madarasa mengi tena kwa namna ambavyo yatadumu. Mengine yamekamilika na mengine bado yanatengezwa,” Moi alisema

Miradi hiyo ni kama ujenzi wa darasa moja katika shule ya kimsingi ya Kimangu (Ksh800,000), ukarabati wa madarasa matatu shule ya msingi ya Kanga (ksh700,000), kujengwa kwa darasa moja katika shule ya msingi ya Ngessumin (Ksh800,000), ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi ya Shalom (ksh 400,000), ujenzi wa darasa moja katika kila shule zifuatazo za msingi, Kayanet, Mogoiwet na Tumaini kwa gharama ya Ksh800,000 kila moja.

Shule za sekondari zilizonufaika ni pamoja na Leldet-ujenzi wa darasa kwa Ksh800,000, Kampi ya Moto, Kandutura na Spring High iliyonufaika na ujenzi wa vyoo kwa gharama ya Ksh 400,000.

“Ua la kuzunguka ofisi za kaunti ndogo ya Rongai liliwekwa kwa gharama ya shilingi 1,217, 656,” aliongeza mbunge huyo.