Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira Alice Chae amekashfu kitendo kilichofanyika mjini Nyamira wakati gavana John Nyagarama alipigiwa makelele mbele ya Rais Kenyatta wakati alipokea kipasa sauti kuhutubia wakazi.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika sherehe ya mazishi katika eneo la Eronge, Chae alisema ni aibu kubwa wakazi kumwaibisha gavana mbele ya Rais, huku akisema huenda gavana huyo alikuwa na jambo la kuomba Rais kutekeleza lakini hakupata fursa ya kuzungumza alichokuwa nacho.
Chae alikashifu kitendo hicho na kuomba ikiwa ni wanasiasa walipanga njama hiyo kuungana na viongozi wote wa Nyamira ili kutafuta suluhu halisi na kutokosa heshima kwa mara nyingine
“Ni aibu wakati kiongozi ananyimwa nafasi ya kuongea kwa kupigiwa makelele mbele ya mheshimiwa Rais Kenyatta,” alisema Chae.
“Naomba wanasiasa wale ambao hawafurahishwi na yale yanafanywa Nyamira kujiunga na viongozi wote kuzungumza badala ya kutumia njia sisizofaa,” aliongeza Chae.
Ikimbukwe kuwa gavana huyo wa Nyamira John Nyagarama na mwakilishi Alice Chae walipigiwa makelele mbele ya Rais na kutopata fursa ya kuhutubia wakazi wakati Rais alikuwa na ziara katika eneo la Kisii.