Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira Alice Chae amesema Wabunge wa upinzani walipinga hotuba ya Rais Kenyatta kuendelea kufuatia uongozi mbaya wa serikali ya Jubilee.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na mwakilishi huyo, serikali ya Jubilee imeshindwa kuzuia ufisadi serikalini haswa kuwachukulia hatua wanaodaiwa kuhusika katika ufisadi huo.

Akizungumza siku ya Alhamisi jioni kupitia redio ya Egesa fm Chae, alisema upinzani uko ili kusinikisha serikali kufanya kazi inavyostahili.

“Ni haki kwa upinzani kukataa udanyanyifu na uongiozi mbaya, ni fursa ya kipekee tulipata kupiga kelele kama njia moja ya kupinga uongozi mbaya,” alisema Chae. 

Chae aliomba serikali ya Jubilee kufanya kazi kwa wakenya haswa kutimiza ahadi ilizotoa mwaka wa 2013 wakati wa kufanya kampeini

Siku ya Alhamisi, Rais Kenyata alipata mda mgumu zaidi bungeni alipokuwa anatoa hotuba kwa wakenya kuzungumzia yale serikali yake imefanya tangu iingie mamlakani na yale itafanya, lakini akapata vikwazo kumaliza hotuba hiyo baada ya baadhi ya wabunge wa upinzani kuzua vurugu.