Wakazi katika kaunti ya Nyamira wameshauriwa  kuwachagua viongozi ambao wataleta maendeleo katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wakazi siku ya Jumapili mjini Nyamira, mbunge wa eneola Mugirango magharibi James Gesami aliwaomba wakazi kutowachagua viongozi wa kupiga siasa tu na kusahau maendeleo ambayo walichaguliwa kufanya.

“Viongozi wanachaguliwa kufanya mendeleo, naomba kila mmoja awe mwangalifu penye anapiga kura katika uchaguzi ujao ili kuchagua viongozi wa meendeleo,” alisema Gesami.

Gesami alikiri yuko tayari kufanyia wakazi wa kaunti hiyo ya Nyamira maendeleo kikamilifu ikiwa atachaguliwa kuwa gavana wa kaunti hiyo.

“Mimi mwenyewe nimekuwa mbunge katika eneo la Mugirango magaharibi miongo miwili na nimeombwa na wakazi nije niwanie ugavana wa Nyamira ili nilete maendeleo na nitafanya hivyo,” aliongeza Gesami.

Wakati huo huo, Gesami alisema kuwa viongozi wa kutofanya maendeleo hawakubaliwi kuchaguliwa, huku akisema mtu huchaguliwa kulingana na mendeleo.