Huenda chama cha KANU kikawasilisha mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao. Haya ni kwa mujibu wa viongozi wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wake Gedion Moi wanaosema kuwa jamii ya Kalenjin imekosa kunufaika vilivyo kupitia serikali ya Jubilee.
Wanasema hawatasubiri hadi mwaka wa 2022 wakati naibu wa rais William Ruto atakapowania urais.
Akiongea na mwanahabari wa radio ya Milele, mgombezi huyo wa urais anadai kwamba kwa miaka tangu waiingie ofisini, Jubilee imekosa kutimiza ahadi zao ambazo walikua wameahidi wakenya kwenye kampeni zao wa mwaka wa 2013.
"Wameweza kutimiza sera zao idadi ndogo sana kupitia yale wakenya walikua wanatarajia kutoka wajumbe hao licha ya matarajio ambayo wapiga kura wao walitarajia," alisema senata huyo wa Baringo.