Chama cha TNA Nakuru kimekanusha madai ya upinzani kwamba hafla ya Jumamosi Afraha ni ya kisiasa. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kaimu mwenyekiti wa TNA kaunti ya Nakuru Harrison Muiruri katika mahojiano Jumatano alisema kuwa mkutano huo wa Jumamosi si wa kisiasa bali ni shukrani kufuatia uamuzi wa ICC kuhusu kesi iliyokuwa inamkabili naibu Rais na mwanahabari Joshua Arap Sang. 

Alisisitiza kuwa wao kama viongozi wa TNA Nakuru wametoa wito kwa wafuasi wao kuwa watulivu na kutojihusisha na siasa siku hiyo. 

"Mkutano huu wa Jumamosi sio wa kisiasa kama wanavyodai wana Cord bali ni hafla tu ya shukrani na kila mtu amealikwa hata wapinzani," alisema Muiruri. 

Wakati uo huo, alipuzlia mbali madai kwamba kuna mgogoro wa uingozi katika afisi ya TNA Nakuru na badala yake kusema kuwa ni propaganda tu ya wachache wasiopenda maendeleo. 

Kiongozi huyo wa TNA Nakuru pia aliwataka wanahabari wa Nakuru kuwa na ufahamu kuhusu chama hicho na uongozi kabla ya kuandika katika vyombo vya habari.

Alikuwa akizungumza baada ya kufanya mkutano na viongozi wa TNA kutoka kaunti ndogo za Nakuru Magharibi na Nakuru Mashariki.