Bila Uhuru na Ruto chama cha JAP kingesambaratika, kulingana na mwekahazina wa chama cha maendeleo ya wanawake kaunti ya Nakuru Florence Chepkorir.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza mjini Nakuru Jumanne, Chepkorir aliwataka watu wa Kaunti ya Nakuru kuiga mfano uliotolewa na wakaazi wa kaunti ya Kericho kwa kudhihirisha alichoita kuunga mkono JAP kwa dhati.

“Sisi wote tunataka kupongeza wapiga kura wa Kericho kwa kuonyesha haki na ukweli ndani ya JAP, na kumchagua Cheruiyot,” alisema Chepkorir.

Chepkorir aliongeza kwamba jamii pana ya wakalenjin haitapotoshwa na yeyote kuondoka ndani ya JAP na ‘kupiga siasa ya kando’.

“Kama jamii ya Kalenjin kutoka Kipsigis, Nandi, Keiyo, Tugen, Marakwet, Pokot hata Wadorobo wako nyuma ya DP Ruto” alisisitiza.

“Sisi tuko ndani ya serikali na hatutaki mtu aje atugawanishe,” akasema bii Chepkorir.

Ushindi wa Aaron Cheruiyot wa JAP katika kinyanganyiro cha useneta wa kericho, umesababisha mhemko mpya katika kaunti ya Nakuru na haswa bonde la ufa, ambayo ni ngome kuu ya naibu rais William Ruto.

Aidha ushindi huo unatarajiwa kufufua upya harakati za JAP kujizolea kura zaidi ikizingatiwa upinzani uliokuwa umeanza kukita mizizi eneo hilo kutoka kwa wabunge na magavana pinzani ndani ya chama cha naibu rais, URP.