Aliyekuwa mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga katika hafla ya awali. [Photo/ nation.co.ke]
Aliyekuwa mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga amewataka Wakenya kupuzilia mbali maandamano ya NASA.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za Jubilee jijini Mombasa, Chidzuga alisema kuwa maandamano hayo yataregesha uchumi wa taifa nyuma.Chidzuga alisema kuwa maandamano hayo hayana msingi wowote bali yatasababisha ukosefu wa usalama nchini.“Maandamano hayo hayana umuhimu wowote kwa taifa bali yatazidi kuibua uporaji wa mali na ukosefu wa usalama,” alisema Chidzuga.Chidzuga amewataka Wakenya kupuuza maandamano hayo na badala yake kufanya harakati zao za kuimarisha uchumi wa taifa kwa manufaa ya siku za usoni.“Musiandamane kamwe, nendeni mufanye vibarua na kazi mupate chakula chenu,” alisema Chidzuga.Aidha, amewasihi Wakenya kutokubali kutumiwa na wanasiasa hasa katika kufanya maandamano ya kuzua fujo.“Musikubali kutumiwa na wanasiasa na kuanza kushambulia jirani yako kwa sababu ya maslahi ya mtu binafsi,” aliongeza.Kauli hii inajiri baada ya mrengo wa upinzani kutangaza kufanya maandamano kila Jumatatu na Ijumaa ili kuhakikisha maafisa wa IEBC wanaodaiwa kuiba kura katika uchaguzi wa August 8 wanapigwa kalamu.