Chifu wa lokesheni ya Rioma iliyoko  eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini Kaunti ya Kisii Oreto Mkurima, amesema atahakikisha upikaji wa pombe haramu umekomeshwa katika eneo hilo

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea mnamo siku ya Ijumaa  katika shule ya upili ya Eramba iliyoko katika eneo hilo wakati wa kuwazawadi wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani  wa kidato cha nne mwaka jana chifu huyo alisema atahakikisha kuwa hakuna mgema wa kupika pompe katika eneo lake  ili wanafunzi wasiharibike kwa kunywa pombe na kukataa kwenda shule.

Wakati huo huo, chifu huyo aliwaomba wazazi kuwalipia watoto wao karo wakati ufaao ili watoto wao wendelee na masomo yao bila taswishi yoyote.

“Nitahakikisha pombe imekomeshwa katika eneo hili maana tukiruhusu upikaji wa pombe haramu  basi tuwe tayari kuona watoto wetu wakiwa walevi kila wakati  jambo ambalo mimi kama chifu wa eneo hili sitakubali kamwe,”alisema Oreto MKrima.

Aidha, chifu huyo aliomba wazazi wale hawapeleki watoto wao shuleni kufanya hivyo kabla hajawachukulia hatua ya kisheria baada ya kukiri kuwa kila mzazi sharti awajibike kwa  mtoto wake kwa kuenda shule maana masomo ni ya bure.

“Naomba kila mzazi apeleke mtoto wake shuleni wale wanajua wazazi wengine kama ni jirani  yako ambaye anakaa na mtoto wake nymbani bila kuenda shule wajulishe kuwa hatari imetangazwa kuwa  msako ukianzishwa atakabiliwa kisheria ,aliongezea Chifu Oreto.