Chifu mmoja eneo la Dundori kaunti ya Nakuru ametishia kufukuza mkaazi aliyehamia huko hivi karibuni kwa madai kuwa yeye na familia yake wataambukiza wanakijiji wengine funza ambazo zimewavamia na kuwashambulia vibaya.

Share news tips with us here at Hivisasa

James Mbugua alihamia Dundori kutoka Kiambu akiwa na familia yake.

Mbugua amedai chifu wa eneo hilo alimwagiza wahame kutoka eneo hilo.

"Niliacha kazi yangu nikaelekea moja kwa moja hadi nyumbani ambapo nilimpata mama aliyejitambulisha Kama chifu Mary Wairimu, na akanieleza kwa ukali kuwa mimi na familia yangu, tulileta funza kutoka tulikotoka, na kuwa anataka tuhame kwa sababu tunaweza kuambukiza wanakijiji wengine,'' Mbugua alisema.

Tayari familia hio imeripoti kisa hicho kwa kamishna wa kaunti ya Nakuru.

Naibu wa Kamishena wa kaunti ya Nakuru, Steven Muchwala alikashifu kitendo hicho na kuahidi hatua zitachukuliwa dhidi ya chifu huyo.

Tayari familia hiyo imeanza kupokea matibabu.