Chifu wa Baharini Nakuru Ali Mohammed amehimza jamii ya kaunti ya Nakuru na wananchi kwa jumla kudumisha amani wakati huu taifa linapokaribia uchaguzi mkuu ujao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza ijumaa katika mkutano wa jamii kuhusu namna ya kupunguza visa vya uhalifu katika jamii,chifu Ali alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwa taifa kushuhudia machafuko tena kutokana na wananchi kusahau yale yaliyotokea mwaka wa 2007/2008 baada ya uchaguzi mkuu.

"Sisi wananchi tuna wajibu mkubwa katika kuhakikisha kwamba maswala ya amani yanaenezwa katika jamii na kamwe hatutaki kurejea katika siku za mwaka 2007 wote tunajua kilichotokea kwa hivyo mie nawarai tu tafadhali tudumishe amani kuanzia nyumbani kwetu"alisema.

Chifu Ali alitoa wito kwa wenye nyumba za kupanga kuhakikisha kwamba wanawatambua wapangaji wa nyumba ili kuepuka migogoro na uhalifu kutekelezwa pasina wahalifu kujulikana.

"Kila mwenye nyumba za kupanga anafaa kuwatambua wapangaji wake na hii itasaidia pakubwa katika kupunguza uhalifu katika jamii hii"alisema.

Wakati huo huo aliwahimiza wazazi kushirikiana na serikali katika kampeni dhidi ya ukambi inayotarajiwa kuanza Jumatatu kote nchini.

Kwa mujibu wake kampeni hiyo ni juhudi za serikali kuhakikisha kwamba inapunguza maambukizi  ya ugonjwa huo kwa watoto wa umri wa miezi 9 hadi  14.

Ni wito ulioungwa mkono na machifu Timothy Kitetu wa Afraha na Jane Muthoni wa Kivumbini.