wakaazi wa wadi ya Gesima, kaunti ya Nyamira wameobbwa  kutouza mashamba yao, kwani yanaleta shida nyakati  zijazo kwa familia, hususani  kwa watoto wao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea hii leo, Jumatatu, kwa balaza la  wakaazi  wa lokesheni ya Mochewa, chifu wa wa eneo hilo, Makori Magara, alisema kwamba mashamba ya yamelete mizozo mingi katika familia, na kwa kiwango kikubwa yamechangia kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa sababu ya mzozo wa fedha.

“Mnapouza mashamba yenu, ni vyema pia mwahusishe wake wenu, ndiyo inaweza zuia mizozo mingi ambayo naripotiwa afisini mwangu,” alihoji chifu huyo.

Wakaazi wengi wa eneo hilo wamekuwa wakihusika na kuuza mashamba yao kwa wawekezaji, jambo ambalo limechangia kwa kesi nyingi.

Aliongezea kuwa uuzaji wa pombe ambao umekithiri katika sehemu hiyo umeharibu maisha ya vijana wengi, huku wengi wakiachana na masomo na kujiingiza katika visa vya unhwaji.

Magara amewaonya kutoendeleza upikaji pombe huo, huku akihapa kuwachukulia hatua za kisheria wagema. 

Wengi wa vijana katika eneo hilo wameingilia unywaji wa pombe, jambo ambalo limekuwa donda dugu kwa nyingi za familia.