Chifu Francis Kariuki wa Lanet ametoa wito kwa vijana kuwa na uzalendo na kudumisha amani has tunapokaribia uchaguzi mkuu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Chifu Kariuki ambaye alitambulika mno kwa kueneza maswala ya amani kupitia mtandao wa kijamii wa twiter alisema kuwa vijana ni nguzo muhimu katika kueneza amani. Alikuwa akizungumza Jumapili katika hafla ya usajili wa watu eneo hilo kupata vitambulisho vya kitaifa kupitia mpango maalumu ujulikanao kama 'Mobile ID Registration'. "Wito wangu Kwa vijana ni kwamba wawe na utulivu na waeneze amani katika sehemu wanazoishi,"alisema.

Wakati huo huo alihimiza vijana na yeyote asiye na kitambulisho cha kitsifa kutumia fursa hiyo.

Kwa mujibu wake, ukosefu wa vitambulisho ni pigo Kwa usalama.

"Inakuwa rahisi kutambua mhalifu akiwa na kitambulisho, lakini akikosa inakuwa vigumu,"aliongeza Chifu Kariuki.

Alitoa wito Kwa wale ambao wako na makosa katika vitambulisho vyao kufika katika afisi husika. Ni vyema kuashiria hapa kwamba serikali ilianzisha mpango huo wa 'Mobile ID Registration' ili kurahisisha usajili wa wananchi kupata vitambulisho vya kitaifa.