Baadhi ya wasichana wadogo wa kurandaranda mjini Eldoret al maarufu chokoraa wanashiriki ukahaba usiku.
Wasichana hao wanadai kuwa waliamua kuanza kutumia mbinu hiyo ili kuimarisha mapato yao baada ya kufurushwa kutoka katikati mwa mji huo na utawala wa jimbo la Uasin-Gishu.
“Si kupenda kwetu kushiriki katika ukahaba bali ugumu wa maisha ndio umetufanya kujiiingiza katika ukahaba,” alisema mmoja wa wasishana hao.
Msichana huyo alidai kwamba mbali na kushiriki katika ukahaba wanapitia changamoto nyingi usiku ikiwa ni pamoja na kunajisiwa na wanaume haswa walinzi wa usiku miongoni mwa matatizo mengine.
Wahudumu wa mapenzi al maarufu makahaba mjini humo walikiri kwamba watoto hao wa kati ya miaka 12 -18 wamejiingiza katika ukahaba.
“Kuna watoto ambao wakati wa mchana wanakuwa chokora usiku wanajirembesha na kuwa makahaba huw atunakutana nao haswa kwenye barabra kuu ya Uganda hapa mjini,” alisema kahaba mmoja
Wasichana husika walidai kwamba wakati mwingine pesa ambazo wanapata kupitia kwa umalaya huchukuliwa na maafisa wa usalama usiku.
“Hata ukiwa umepata pesa kidogo wakati mwingine unawezapoteza kila kitu haswa wakati polisi wanapotushika inabidi ujitetee na pesa ili uachiliwe la sivyo utapelekwa jela uozee huko,” alisema chokora mmoja
Tayari baadhi ya wasichana hao wanaishi na virusi vya ukimwi ambavyo husababisha ugonjwa wa ukimwi.
“Mimi hivi ukiniona hivi nina virusi vya ukimwi kupata dawa ni shida,chakulanayo hivyo hivyo sasa sisi hatujui tutaenda wapi na watoto wetu,” alisema
Kutokana na hali hiyo shirika la kuhudumia watoto katika jimbo la Uasin-Gishu limesema litaanzisha ushauriano na wadau wengine kutafuta mbinu bora ya kuwanususru watoto hao.