Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Chache kaunti ya Kisii ambaye pia ni mwanakamati wa pesa katika bunge la kitafa Richard Tong’i amesema atahakikisha chuo kikuu cha Kisii kimeongezewa kiasi cha  pesa ambazo hutoka kwa serikali kuu ili chuo hicho kuendelea na masomo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumanne katika eneo la Kiogoro eneo lililoko eneo bunge lake mbunge huyo alisema miongoni mwa vyuo vikuu hapa nchini chuo ambacho hupokea pesa kidogo zaidi ikilinganishwa na vyuo vingine  kutoka serikali ya kitaifa ni chuo kikuu cha  Kisii na kusema atahakikisha pesa hizo zimeongezwa hadi kiwango vyuo vingine hupokea hapa nchini.

“Chuo kikuu chetu cha Kisii kina wanafunzi wengi sana kama vyuo vingine lakini ndicho hupokea pesa kidogo kutoka serikali kuu nikienda tukiwa na kikao na wanakamati wengine wa bunge la Kitaifa nitajaribu chuo chetu kiongezeawe pesa,” alisemaTong’i

“Chuo chetu kikipokea pesa nyingi wanafunzi wetu watapata masomo kwa kiwango kinachostahili ili waje kujisaidia nyakati zijazo,” aliongeza Tong’i.

Aidha mbunge huyo alisema chuo cha Kisii kinafanyiwa ufisadi wakati hakipokezwi pesa kama vyuo vingine hapa chini na kuomba serikali kuu kutobagua vyuo vingine na vbiko na weanafunzi wengi .

“Pesa zikiongezwa kwa chuo chetu cha Kisii hatutakuwa na lolote la kugombanisha serikali kuu wakati huu chuo cha kisii nitahakikisha kimepata pesa sawia na vyuo vingine ,” alisisitiza Tong’i