Chama cha Wafanyibiashara wanaoagiza magari kutoka nchi za nje (Car Importers Association of Kenya) CIAK, kimeunga mkono juhudi za Mamlaka ya ushuru nchini KRA, kuyasaka makasha yenye bidhaa za magendo katika Bandarini ya Mombasa.
Mwenyekiti wa Chama hicho, Peter Otieno, alisema kuwa hatua hiyo itasaidia pakubwa kuzuia uingizaji wa bidhaa za magendo na gushi nchini, ikiwemo magari, sukuri, mchele na biadhaa zingine ambazo zinazorotesha shughuli za kibishara.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Otieno alisema kuwa tabia ya baadhi ya wawekezaji kukwepa kulipa ushuru imekuwa desturi nchini.
Alisema kuwa hali hiyo imesababisha kudidimia kwa uchumi wa nchini pamoja na kuhatarisha maisha wa Wakenya wanaotumia bidhaa hizo.
Otieno aliitaka Mamlaka ya KRA kuzidi kuendeleza oparesjheni ya kukamata makasha yenye bidhaa za magendo, na kusisitiza kuwa mamlaka hiyo inapaswa kuangazia zaidi hata upande wa uingizaji magari, kwani baadhi ya wafanyibiashara wanatabia kama hiyo.
"Tunapongeza hatua ya Mamlaka ya Ushuru nchini KRA, kwa kuendeleza oparesheni kali ya kusaka makasha ya bidhaa za magendo, kwani wafanyibiashara wengi wanakwepa kulipa ushuru,” alisema Otieno.
Kauli ya Mwenyekiti huyo wa CIAK inajiri baada ya maafisa wa Mamlaka hiyo kukamata kasha lililokuwa na magari matatu ya kifahari yalioingizwa humu nchini kupitia Bandari ya Mombasa kwa njia ya magendo, ili kukwepa kulipa ushuru.