Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini CIPK, imeitaka Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwanyima vibali vya kuwania uongozi wanasiasa wanaokabiliwa na kesi za uchochezi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katibu mshirikishi wa baraza hilo Sheikh Mohamed Khalifa amesema hatua hiyo itahakikisha viongozi nchini wanaasi siasa potovu za uchochezi.

“Hatua hiyo itaweza kupunguza idadi ya viongozi wanaoeneza chuki kwa jamii,” alisema Khalifa.

Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona viongozi wakitoa matamshi ya uchochezi ambayo yanaweza gawanya wananchi.

“Kila siku wanasiasa wakiwa jukwaani wanatoa matamshi ya uchochezi yasiyokuwa na manufaa kwa raia,” alisema Khalifa.

Aidha, ameitaka Wizara ya Usalama kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wanaoendeleza ukabila na chuki.

Wakati huo huo, amelitaka jopo linalo endeleza ukaguzi wa makamishna wapya wa IEBC kufuata katiba na kutoingiza ukabila katika uteuzi huo.