Ikiwa muungano wa upinzani Cord unahitaji kupea serikali iliyoko mamlakani tumbo joto kisiasa katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017, muungano huo unafaa kutoa mwaniaji urais tofauti kando na kiongozi wa muungano huo Raila Odinga ambaye amejaribu mara tatu bila mafanikio.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na maoni kutoka kwa wakaazi wa kaunti ya Kisii Raila hastahili kusimama tena katika kiti cha urais ila kuunga mkono mmoja wa vigogo wa muungano huo wa Cord ili kubuni ushindi.

Wengi walipendekeza kuwa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo musyoka anafaa kuwa mwaniaji wa urais kupitia muungano wa Cord ili kumenyana  na mrengo wa Jubilee kwani huenda uwaniaji wake ukatikisa kambi ya Jubilee.

Pia wakaazi hao walisema kuwa kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula hatatosha mboga kwa mrengo wa Jubilee kwani hajulikani sana kisiasa kama Kalonzo

Kulingana na wakaazi hao Wetangula anafaa kuunga mkono Kalonzo Musyoka kwa kuwa naibu wake.