Mrengo wa Cord umetangaza kuanza maandamano yake ya amani kuanzia jumatatu wiki ijayo.
Sababu ya maandamano hizi ni kushinikiza kuondolewa ofisini kwa makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Mwenyekiti wa ODM, John Mbadi alisema maandamano hayo yataendelea licha ya amri ya mahakama kuupinga akidai hawakuwa wamehusishwa katika kesi iliyowasilishwa na baadhi ya wabunge wa jubilee.
Aidha, wafuasi wa mrengo wa Cord kote nchini watafanya maandamano katika kila ofisi za IEBC ili kushinikiza kutimuliwa kwa makamishna wa IEBC na maafisa wapya kuteuliwa kusimamia uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2017.