Vinara wa Cord wakiongozwa na Raila Odinga, wamejitokeza kuonyesha kutoridhishwa kwao na uongozi wa serikali ya Jubilee.
Vinara hawa akiwemo aliyekuwa makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na senator wa kaunti ya Bungoma Moses Wentangula wameilaumu Jubilee kwa kutotimiza ahadi ilizowapa Wakenya.
Raila alisema kwamba Jubilee imezorotesha hali ya uchumi hadi sasa wananchi wanatumia kiasi kikubwa cha fedha kugharamia chakula, nyumba na mavazi.
"Ikilinganishwa na mwaka wa 2012, hali ya maisha imekua ghali sana. Maziwa sasa inauzwa na shilingi 60. Hapo awali ilikua shilingi 45 kwa lita," Raila alisema.
Kwa upande wake, seneta Wetangula amelalamikia hali mbaya ya amani nchini huku Kalonzo akishutumu IEBC.
Mrengo wa Cord umemsuta rais Uhuru Kenyatta na serikali yake kwa kuwandanganya Wakenya. Haya yanajiri wiki moja baada ya hotuba ya rais kwa bunge la kitaifa na lile la seneti kuhusu hali ya nchi.