Muungano wa Cord ukiongozwa na vinara wake Raila Odinga na Moses Wetangula pamoja na wafuasi wao, jumatatu walifurushwa nje ya Anniversary Towers baada ya kuzua rabsha wakilenga kuwatimua makomishina wa tume huru ya uchaguzi, IEBC afisini mwao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi ili kuwatawanya baada ya kutaka kuingia kwenye jengo hilo kwa mabavu.

Cord imekua ikishinikiza kwamba tume hiyo ya IEBC imekua ikifanya kazi kwa upendeleo mkubwa. 

Wanadai kua IEBC ni tume iliyosheheni ufisadi na mapendeleo kwa hivyo uchaguzi wa mwaka ujao hautakua wa haki.

Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri alisema kwamba hatua ya Cord ya kutaka kuitimua IEBC ni jambo la aibu na linafaa kuadhibiwa.

“IEBC haipigi kura, ni wananchi ndio wanapiga kura kwa hivyo Cord kutaka kufurusha IEBC haina maana yoyote. Ni jambo la aibu kwao na wafuasi wao,” alisema Ngunjiri.