Dereva wa trela amefariki huku taniboi wake akinusurika baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya katika barabara ya Mau Summit kuelekea Londiani.
Trela hiyo ambayo ilikuwa imebeba mizigo kutoka Mombasa kuelekea Kisumu ilipoteza mwelekeo kabla ya kubingiria mara kadha.
Kulingana na Joseph Ongeri ambaye ni taniboi, huenda breki za trela hiyo zilifeili na kupelekea ajali hiyo.
Madereva wanaotumia barabara hiyo wameuliza serikali pamoja na wanakandarasi wanaokarabati barabara hiyo kuweka alama za barabara pamoja na matuta ili madereva wapunguze mwendo.
Aidha wanaotumia barabara hiyo wameuliza madereva kuwa wangalifu na kuheshimu sheria za trafiki ili kupungaza ajali.