Ulimwengu unapoadhimisha siku ya maji mwaka huu, mwakilishi wa zamani wa eneo wadi la Nyamira mjini Paul Kengere amejitokeza kulalamikia vikali utoaji huduma za usambazaji maji katika kaunti  hiyo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye mahojiano mapema Jumanne, Kengere alilalamikia kutosambazwa maji kwa wakati unaofaa, huku akidai wakazi wa kaunti ya Nyamira huuziwa maji kwa shillingi ishirini kwa mtungi wa lita ishirini wa maji kinyume na inavyotarajiwa. 

"Kwa muda sasa huduma za usambazaji maji katika kaunti hii zimekuwa mbaya na zisizotegemewa kwa maana maafisa wa usambazaji maji husambaza maji kwa mgao huku ikitulazimu kununua mtungu wa lita ishirini wa maji kwa shillingi 20," alilalama Nyamweya. 

Nyamweya aidha alisema kwamba pesa zilizotengewa idara ya maji hazijakuwa zikitumika vizuri, kwani kwa muda sasa pampu za usambazaji maji zilizochakaa na kuharibika hazijabadilishwa.

"Pampu za usambazaji maji zilizoezekwa ardhini miaka mingi iliyopita ili kusambaza maji hazijabadilishwa, huku zingine zikipasuka, hali inayosababisha ukosefu wa usambazaji maji huku Nyamira, na ndio maana sharti gavana Nyagarama awachukulie hatua maafisa wa idara ya maji," aliongezea Nyamweya.