Makao makuu ya tume ya EACC.[Picha/ standardmedia.co.ke]Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi EACC tawi la Mombasa, imewasilisha faili ya naibu mkuu wa kituo cha polisi cha Kiembeni John Shikondi kwa afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.Haya yanajiri baada ya Shikondi kutiwa mbaroni kwa madai ya kuitisha hongo ya shilingi elfu nane.Msemaji wa tume ya EACC Yasin Amaro alisema wanashirikiana na taasisi husika ikiwemo mamlaka ya usalama barabarani NTSA kumfungulia mashtaka afisa huyo.“Tutashirikiana na taasisi zingine ili tuweze kumfungulia mashtaka afisa huyo,” alisema Amaro.Shikondi alitiwa mbaroni katika mkahawa mmoja eneo la Bamburi baada ya kuekewa mtego na maafisa wa tume ya EACC.Polisi huyo alipokonywa silaha yake na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilindini kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50.Amaro alisema kuwa tume hiyo imekuwa ikipokea malalamishi dhidi ya afisa huyo. Alisema kuwa afisa huyo anadaiwa kuwazuilia wananchi bila kuwafungulia mashtaka na kuwapeleka mahakamani.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6
MOMBASA
EACC kumfungulia mashtaka afisa mkuu wa polisi
ADVERTISEMENT
Share news tips with us here at Hivisasa
Thank you for reading my article! You have contributed to my success as a writer. The articles you choose to read on Hivisasa help shape the content we offer.
-Osman Suleiman