Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi EACC, kwa ushirikiano na Tume ya Mshikamano na Ushirikiano wa Kitaifa NCIC, imetakiwa iwachukulie hatua za kisheria viongozi waliyokosa maadili na nidhamu kwa Wakenya.

Akizungumza na wanahabari mjini Nakuru siku ya Jumamosi, kaimu Mwenyekiti wa chama cha TNA Kaunti ya Nakuru Dkt Abdul Noor amezitaka tume hizo husika kuwachukulia viongozi hao hatua za kinidhamu, ili iwe funzo kwa viongozi wengine wenye tabia za kuwatusi viongozi wenzao.

kutokana na tukio ambalo Seneta wa Kaunti ya Machakos Johnstone Muthama kudaiwa kumtusi Rais Uhuru Kenyatta pamoja na Waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru, Dkt Noor amewataka Wakenya kutowachagua viongozi wenye maadili mabaya.

“Tabia ya aina hiyo huenda ikawagawanya Wakenya kwa misingi mbalimbali. Seneta wa Machakos hafai kuchaguliwa tena wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2017,” alisema Noor.

Matamshi haya yanajiri baada ya Seneta Muthama kujiwasilisha mbele ya tume ya NCIC siku ya Jumatano, huku tume hiyo ikiendelea na uchunguzi kuhusiana na matamshi aliyoyatoa wakati wa mkutano uliyandaliwa na muungano wa Cord tarehe Septemba 23.