Kuelimishwa kwa watoto katika jamii kutachangia pakubwa katika hatua za kupunguza maambukizi na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi katika jamii eneo la Nyakach kaunti ya Kisumu.
Hii ni kauli yake pasta Paul Ochola wa kanisa la House of Hope chapel mjini Katito wilayani Nyakach ambaye alisema kupitia kwa elimu vijana watapata kufahamu athari za ugonjwa wa Ukimwi.
Kadhalika, pasta Ocholla alitoa wito kwa wanafunzi kuzingatia zaidi elimu na kujiepusha kabisa na maswala ya utu uzima ambayo kwa sasa hayana manufaa kwao.
Amesisitiza kuwa kupitia kwa masomo changamoto zinazokumba jamii zitapata uvumbuzi wa haraka utakaokuwana manufaa ya kizazi cha leo na jadi.
Akihutubu kwenye mkutano wa maombi kwa wanafunzi pasta Ocholla alisema: ‘’Kuna haja kubwa kwa kila mwanafunzi kujishirikisha na mambo yanayoendana na maisha yake kama mwanafunzi ili kujijengea maisha mema katika siku za baadae.’’