Mwakilishi mteule anawakilisha walemavu katika bunge la kaunti ya Nakuru Emma Mbugua anasema kuwa atawasilisha mswada wa walemavu katika bunge la kitaifa baada ya mswada wa jinsia kutopitishwa.
Bi Mbugua alifichua kuwa elimu ndio chanzo kikuu kilichotatiza kupitishwa kwa mswada huo na bungekuu, kwani mswada huo ulijumuisha vijana, kina mama na walemavu kwa jumla.
Sasa Bi Mbugua anamtaka mwakilishi wa walemavu katika bunge la kitaifa Isaac Mwaura kushirikiana naye ili kuleta mswada wa walemavu pasipo kujumuishwa na ule wa jinsia.
"Niko katika harakati za kutayarisha mswada huo unaolenga walemavu nchini na nitakapokamilisha, nitaupeleka katika bunge letu ili kujadiliwa,na ni matumaini kuwa bunge la kitaifa litaupitisha," alisema wwakilishi huyo
Mbugua, aidha, aliwakashifu wabunge kwa kutouelewa mswada wa kijinsia kwani ulikusudia kuleta mwanamke katika sura mpya ya uongozi.
"Mwanamke si chombo cha nyumbani na tunaweza ongoza taifa pasipo na tashwishi kinyume na wanaume , hisia za mwanamke humshuku na kumfanya mgumu kuingia katika mambo yasiyo kadri na jamii kama vile kupokea rushwa na udanganyifu."