Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Eneo la Pwani litaimarika zaidi kwenye sekta ya utalii pamoja na uchumi huku sherehe za utamaduni zikianza rasmi hii leo, Alhamisi katika Kaunti ya Lamu ambazo ni sherehe hufanyika kila mwaka zikiangazia utanagamano na mila za wakazi.

Haya ni kulingana mwenyekiti wa shirikisho la kushughulikia masuala ya Utalii katika Kaunti ya Lamu Ghalib Alwy, aliyesema sherehe hizo zitainua utalii na uchumi si tu Lamu bali Kaunti zote sita za eneo la Pwani, ikiwemo Mombasa.

Akiongea siku ya Jumanne wakati wa maandalizi ya hafla hiyo, Ghalib alisema kuwa wakazi na wazawa wenye asili ya Kaunti Lamu ambao wanaishi katika Kaunti nyingine watasafiri kwa idadi kubwa, hata wale ambao si wazawa wa eneo hilo huwa wanahudhuria kwenye hafla hiyo kila mwaka.

Aidha, aliongeza kusema kuwa sherehe hizo zimekuwa zikitandawaa kwa umarufu, na katika miaka ya hivi karibuni, hafla hizo zimekuwa zikiwapokea watalii kutoka nchi za ulaya na Marekani pamoja na watalii kutoka nchini ambao wamechangia kuinuka kwa viwango vya kibiashara.

Sherehe hizo zitaendelea kwa siku nne na zinahusisha maonyesho ya kitamaduni kama vile kunengua viungo, kupanda punda, akiwa mnyama ambaye hutumiwa na wenyeji kusafirisha bidhaa zao za sokoni na hata kwa uchukuzi binafsi.