Msanii aliyetambulika sana kwa kibao chake cha kaka Saidi Escoba sasa ameanza kurudi kwenye vinywa vya wanaopenda burudani kutoka pwani kutokana na miziki anayoendelea kuachilia.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwezi jana Escoba aliaandaa tamasha la radio lililomlazimu kuzuru zaidi ya vituo kumi kote nchini vya radio ili kuuza mziki wake ili aweze kuchukua nafasi yake ya jadi katika tasnia ya miziki hapa pwani na nchini kote kwa ujumla.

Akichonga moja kwa moja kwenye mahojiano baada ya kuwa miungoni mwa wasanii waliotumbuiza umati uliofurika wakati wa hafla ya mwanasiasa tajika hapa pwani wiki jana.

Anasema baada ya kuamua kurudi chuo na kujihusisha na biashara nyenginezo, tamaaa kuendelea na biashara ilimjaa asijue alichokuwa anapoteza kutokana na kipaji alichojaliwa na sasa ameahidi kutowabwaga wafuasi wake kwenye matamasha yote anayotarajiwa kutumbuiza mwezi huu wa Disemba.

Esco ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wakifanya vyema hapa pwani wakati wa mwanzo wa safari na kina Yusuf Kombo maarufu kama Susumila na ingelikuwa ni uadilifu katika tasnia hiyo ya uaimbaji basi huenda akawa yupo mbali kimziki kanda ya Afrika mashariki.

Kwa sasa amezidi kutwaa viingi ya vituo vya burudani hapa pwani hasa baada ya kuwashirikiana na vijana wengi wanaochipuka huku akiahidi mashabiki wake kuwa mengi yapo jikoni na yatakamilika mwezi huu wa Disemba.