Familia kadhaa katika kijiji cha Michatha eneo bunge la Molo zinakadiria hasara baada ya nyumba zao kuteketezwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Nyumba hizo ziliteketezwa Jumanne baada ya moto kuzuka kwenye eneo hilo. Moto huo unadaiwa kusababishwa na hitilafu za nguvu za umeme.

“Miti ya stima ilianguka na kusababisha moto huo. Watu wengi wameathirika kwa kuwa ulivuma kwa kasi na ikawa ngumu kuokoa mali,” John Kimani alisema.

“Wengi wa wakaazi walikuwa kwenye shughuli zao, ndio ikawa vigumu kutoa vitu za nyumba,” Jecinta Wambui alisema.

Hakuna majeraha wowote ambao waliripotiwa kwenye kisa hicho.