Familia ya mshukiwa Mohamed Sudi anayedaiwa kuhusika na mauwaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la waislamu, CIPK, marehemu Sheikh Mohamed Idris imepinga hukumu ya kifo iliyopewa kijana wao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongozwa na Ayub Athuman Warisanga kaka wa mshukiwa, imesema inapinga uamuzi wa mahakama na itakata rufaa ili haki ipatekane kwa mpendwa wao.

Siku ya Ijumaa, Warisanga ,ametofautiana na hukumu hiyo na kuitaja kuwa ya kukandamiza haki za raia wasiokuwa na hatia.

Haya yanajiri muda mchache tu baada ya mahakama kuu jijini Mombasa kumuhukumu kifo mshukiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la waislamu, CIPK, marehemu Sheikh.

Mnamo Juni 10, 2014, Mohamed Soud anadaiwa kuhusika katika mauwaji ya marehemu Mohamed Idris katika eneo la Likoni.

Siku ya Ijumaa, jaji Martin Muya alisema kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka unaonyesha wazi kuwa mshukiwa ndie aliyehusika pakubwa katika kumpiga risasi hadi kufariki sheikh Idris.

Mshukiwa yuko na siku 14 za kukata rufaa.

Mwezi Disemba mwaka jana, Soud, aliwalaumu maafisa wa usalama kwa kumuhusisha na mauwaji hayo, umiliki wa bunduki na kilipuzi, ikizingatiwa hana ujuzi wa kutumia silaha hizo hata kidogo.