Familia tisa katika eneo la Mtongwe, Kaunti ya Mombasa, zimeachwa bila makao baada ya moto kuteketeza makaazi yao siku ya Jumapili.
Moto huo uliteketeza nyumba hizo kwa kasi, huku wakaazi wakilazimika kutumia mbinu duni kuuzima, hasa baada ya wazima moto wa kaunti kufika katika tukio la mkasa huo wakiwa wamechelewa.
Kufikia sasa, chanza cha moto huo bado haujabainika, licha ya kuwepo na tetesi kuwa moto huo ulisababishwa na hitilfu za umeme.
Familia zilizoathirika zimepata hifadhi katika kanisa la Deliverance lililoko katika sehemu hio.
Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho aliwasili katika eneo la mkasa huo na kuzifariji jamii zilizoathirika.
“Ningependa kuwapa pole waliokutwa na mkasa huu, na kuwashukuru waliotoa msada kwa waathriwa, hasa kanisa la Deliverence lililotoa malazi kwa waathiriwa,” alisema Joho.
Joho aliahidi kuwasaidia waathiriwa wa mkasa huo na mahitaji muhimu ili kuwawezesha kuanza maisha upya.
Baadhi ya waathiriwa wameshtumu serikali ya kaunti kwa kutokuwa na vifaa vya kutosha katika kukabiliana na mikasa ya moto.