Familia ya marehemu Akasha imeitaka serikali kuelezea waliko wana wao wawili pamoja na raia wawili wa kigeni waliokamatwa na maafisa wa polisi siku ya Jumamosi.
Wanne hao walikamatwa nyumbani kwao eneo la Nyali, na hadi sasa hawajulikani waliko. Tetesi zasema kuwa huenda wakasafirisha hadi nchini Marekani kufunguliwa mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Ibrahim Akasha, Gulam Hussein, Vijaygiri Goswami na Baktash Akasha wanakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa dawa za kulevya katika mahakama ya Mombasa.
Ikumbukwe wanne hao wanahitajika nchini Marekeni baada ya kuhusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Wakili wao Cliff Ombeta alisema kuna njama ya serikali kujaribu kukandamiza haki za wateja wake kwa kuwahusisha na kasha la mihadharati lililonaswa bandarini Mombasa.