Mzee mmoja kutoka kijiji cha Ebiosi Kiamokama, Wilaya ya Masaba Kusini katika Kaunti ya Kisii ameiomba Serikali ya Kaunti hiyo kumsaidia kulipa mikopo aliyokopa kutoka kwa mashirika mbalimbali.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea na mwandishi huyu wa habari siku ya Jumatano, Mzee huyo kwa majina Joseph Obare alisema kuwa ana changamoto chungu nzima baada ya kumpoteza mwanaye kwa jina Joash Obare Mosira, ambaye ni kitinda mimba katika familia yake, aliyefariki katika Chuo cha Garissa kilichoshambuliwa na kikundi cha wanamgambo Al-Shabaab siku ya Alhamisi.

Haya yanajiri baada ya Obare kumpoteza kijana wake aliyekuwa tegemeo lake kwa siku zijazo kwani alikuwa akikopa mikopo mingi kutoka mashirika mbambali ili kumsomesha mwanawe akiwa na matumaini kuwa angemsaidia kulipa mikopo hiyo baada ya kumaliza masomo kwani alikuwa amebakisha mwaka mmoja tu katika Chuo hicho ili akaweze kuitimu, lakini kwa bahati mbaya akauawa.

“Naomba Serikali ya Kaunti yetu ya Kisii inisaidie kulipa mikopo ninayo kwa sasa maana niliyemtegemea kunisaidia kulipa ameaga dunia na sina kuingine pa kutoa hizo pesa na tayari nimekumbwa na mauti katika familia yangu baada ya mtoto wangu kufariki katika shambulizi la Garissa,” alihoji Obare.

Familia hiyo inahitaji usaidizi kutoka kwa Serikali kushirikiana pamoja katika mazishi ya mwanao, ikumbukwe kuwa Kaunti ya Kisii ikiongozwa na Gavana James Ongwae aliahidi hapo mbeleni kulipotokea shambulishi hilo hapo siku ya Jumapili kuwa Serikali yake itafanya kila iwezalo ili kuakikisha familia zile zilipoteza wenzao zimeshughulikiwa kikamilifu.

Ombi kubwa la Mzee Obare ni kusaidiwa na Serikali ili kuakikisha kwamba juhudi za kusaidiwa kulipa mikopo zimehitimizwa ikiwezekana.