Familia moja katika kijiji cha Kimasare wilaya ya Nyamira kusini wana hofu ya mtoto wao ambaye amepotea kwa mda wa mwezi mmoja sasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Jeff Onsomu, (10), wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Maua, Naivasha yasemekana amepotea tangu tarehe 11 mwezi wa nne mwaka huu baada ya yeye kwenda kucheza na wezake na hakurudi.

Kulingana na dadake aliyekuwa anaishi na Onsomu, kakake alitoka nyumbani akiwa na furaha akielekea kucheza na rafikize kwa kuwa walikuwa washa funga shule, na hajarejea tangu siku hiyo.

Mamake Onsomu alisema kwamba imekuwa kazi ngumu ya kumtafuta mwanake muda huu wote bila kumpata, na akaongeza kwamba mwanaye hana kasoro ya upungufu wa akili hata kidogo.

"Swala hili halinipatii usingizi hata kidogo kwa kuwa huyu mtoto hajawai potea wala kuwa na tatizo la akili pungufu, naomba yeyote aliye na habari kumuhusu awasiliane nasi ili kutupunguzia mawazo," alisema mamake.

Kijana alikuwa amevaa nguo nyeusi na mabupanzi katika siku hiyo ya kupotea, na kupotea kwake kuliripotiwa katika kituo cha polisi cha Kongoni.

Mamake mtoto anaweza kufikiwa kwa nambari 0714070649.