Kivuko cha feri cha Likoni. [Picha/ the-star.co.ke]
Halmashauri ya Huduma za Feri (KFS) nchini imesema feri mpya ijulikanayo kama MV Jambo iliyotengenezewa nchini Uturuki, itawasili nchini tarehe 27 mwezi ujao.
Feri hiyo itahudumu katika kivuko cha Likoni.Mkurugenzi Mkuu wa KFS Bakari Gowa amesema feri hiyo iliyozinduliwa rasmi nchini Uturuki kwenye sherehe iliyohudhuriwa na maafisa wakuu wa serikali kutoka humu nchini inatarajiwa kuanza safari yake tarehe Julai 6 kuja mjini Mombasa.Gowa amesema kwamba anaimani kuwa wakaazi wanaotumia kivuko cha feri cha Likoni watanufaika na huduma za feri hiyo itakapowasili humu nchini.Kulingana na Gowa, feri hiyo mpya iko na urefu wa mita 84.6, upana wa mita 18 na itakuwa na uwezo wa kubeba uzito wa tani 1,534.MV Jambo ni mojawapo ya feri mbili ambazo serikali ya Kenya imeagiza kutoka Uturuki kwa Kima cha shilingi bilioni 2.2.