Chama cha Ford People kimeanza mikakati ya kujiunga na chama cha Jubilee.
Hii ni baada ya chama cha Jubilee kutaka vyama vingine kuvunjwa na kuunda chama kimoja.
Akizungumza siku ya Jumatano, katibu wa chama hicho cha Ford People katika kaunti za kisii na Nyamira Albert Nyaundi wamefanya mazungumzo ya kuingia Jubilee.
“Chama cha Ford People kimekubali kufanya mazungumzo na chama kipya cha Jubilee jinsi wataungana pamoja na kupiga siasa pamoja kisha baadaye kuleta maendeleo,” alisema Albert Nyaundi.
Aidha, Nyaundi alisema chama hicho chao ingawa kitaungana na Jubilee sharti kwanza viongozi wapya wateuliwe baada ya viongozi waliokuwa wanakiendesha chama hicho muda wao ulikamilika disemba mwaka jana lakini wanaendelea kushikilia hadi viongozi wapya kuteuliwa.