Wazee wa vijiji katika lokesheni ya mochenwa wadi ya Gesima wameombwa kuwaelimisha wakazi kuhusu umuhimu wa mradi wa nyumba kumi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea hiyo jana  katikaka ofisi yake naibu wa chifu wa lokesheni ya Mochenwa wadi ya Gesima eneo bunge la Kitutu masaba kaunti ya Nyamira Richard Makworo aliwaomba wazee kuelimisha wakazi kuhusu umuhimu wa mradi wa nyumba kumi.

Aidha alisema kuwa hiyo ndio njia moja ya kusaidia wakazi hao kufahamu vyema malengo na nia ya mradi huo  wa serikali haswa kumaliza ugaidi.

“Ni muhimu kila mkazi kuelewa umuhimu wa mradi huu ili kutusaidia katika kudumisha usalama kwani  kila mtu akijua jirani  yake mambo ya usalama yatakuwa shwari,”alisema Makworo

Wazee hao ambao walikuwa katika ofisi hiyo kwa hafla ya kuzungumzia suala la usalama katika lokesheni hiyo wakiongozwa na mzee Nyakwana Orogo kutoka kijiji cha Kiamitengi alisema kuwa watahakikisha kuwa wakazi wote wamepokezwa mafunzo ili kujua umuhimu wa mradi huo.

Mzee nyakwana ,aliwaomba wenyeji kuhakikisha kuwa wamewatabua watu wanaowajiri katika boma zao.

Nyakwana pia alipendekeza kuwa machifu wanapswa kuwapatia barua watu wa maeneo yao wanapoenda kutafuta kazi katika lokesheni zingine.

Wakazi katika lokesheni hiyo wamekuwa wakishudia visa vya wizi kwa muda mrefu na kuwalazimu machifu kushughulikia jambo hilo kikamilifu.

Kulingana na makworo watu wakifahamu vyema umuhimu wa mradi huo wizi utapungua katika eneo hilo.