Mgombeaji wa zamani wa kiti cha ubunge katika eneo la Bobasi Samson Moracha ameshtumu wasimamizi wa pesa za wakongwe, baada ya zoezi la juzi lililotibuka kutokana na hitilafu ya mtandao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Moracha, ambaye amewahi aligombea kiti hicho mwaka wa 2007, alistaajabu kuona kina nyanya na kina babu wakiwa wameshikiliwa mikono huku wakingoja pesa kutoka kwa serikali siku ya Jumanne, ambapo watu wachache tu walilipwa huku wengine wakiambiwa warejee mwisho wa mwezi.

Moracha alikuwa akiongea baada ya kuzuru uwanja wa Gusii kujionea maendeleo ya ujenzi wa uga huo.

“Si vizuri hata kidogo kuweka wakongwe hawa kwa mda mrefu kiasi hicho na kuwaambia waje baadaye, si haki hiyo na wengine wamezeeka sana,” alihoji Moracha.

Kiongozi huyo aliahidi kulishughulikia swala hilo, ili kuhakikisha njia mwafaka inapatikana ya kuwalipa wakongwe hao.

Hata hivyo mmoja wa maafisa kutoka benki ya KCB, ambayo ilihusika kuwalipa wakazi hao, alisema kuwa kulitokea hitilafu za kimitambo ambayo ilisababisha kucheleweshwa kwa shughuli hiyo.