Gari moja la usafiri lilivamiwa huku mali ya takriban elfu mia mbili kuibiwa na majambazi waliojihami katika eneo la Soilo barabara ya Nakuru kuelekea Njoro mapema Jumanne asubuhi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Michael kirui, ambaye ni dereva wa lori hilo la kampuni ya Bunda cake and feeds Limited, alivamiwa na majambazi hao alipokuwa akiingia mjini kutoka kwake njoro alikolala baada ya kupeleka bidhaa jana katika eneo la Kapsabet majira ya saa mbili unusu asubuhi

Amesema kuwa gari la aina ya probox lilimzuilia njia, huku jamaa mmoja aliyekuwa juu ya pikipiki akimlenga na bastola

Amesema kuwa aliamrishwa kuweka gari kandokando mwa barabara, huku akitakiwa kutoa hela zote alizokuwa nazo sawia na simu yake ya rununu.

Hata hivyo, amedokeza kuwa  huenda wakora hao wanamfahamu kwa misingi walimwamrisha kwa jina lake.

Vilevile. imebainika kuwa ni wiki jana tu dereva ambaye alikuwa akiliendesha gari hilo alipopigwa risasi  na kuaea alipokuwa akiingia katika makazi yake katika eneo la Mwariki viungani mwa mji wa Nakuru

Hata hivyo, Geofrey Kamau, ambaye ni msimamizi wa kampuni husika amesema kuwa  huenda wakora hao wanalenga gari za kampuni yao, akiongeza kuwa visa hivyo vyote vimeripotiwa kwa polisi na hakuna hatua ambayo imechukulwa.

Kamau amedokeza kuwa tangia Januari, kampuni yao imepoteza takriban shilingi 500,000 kwa visa vya aina hiyo, huku akiitaka idara ya usalama kuimarisha usalama hasaa katika barabara kuu sawia na kuchunguzs magari ya aina ya probox.

Hata hivyo. juhudi za kuongea na OC PD wa Nakuru hazikufua dafu.