Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa Kaunti ya Mombasa amesema kuwa ana matumaini kuwa kiwango cha pesa za ‘Xmass Tree Fund’ kitaongezeka mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana.

Sherehe hizo al maarufu kama 'Governor’s Christmas Tree', huandaliwa kila mwaka na zilifanyika siku ya Alhamisi katika Ukumbi wa Kaunti ya Mombasa, lengo kuu ikiwa ni kuchangisha fedha kwa watoto wanaotoka katika familia zisizojiweza.

Akiongea wakati wa sherehe hizo, Gavana Hassan Joho alisema wana matumaini kwamba mwaka huu watachangisha pesa nyingi zaidi.

“Mwaka jana tulichangisha shilingi milioni 10 pesa ambazo zilisaidia maelfu ya watoto kuendelea na masomo yao. Mwaka huu tuna matarajio makubwa na tunaomba watu wote washirikiane,” alisema Joho.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Ijumaa, Mary Wairimu, mzazi alisema kuwa wazazi wamefurahishwa na hatua hiyo ya gavana ya kusaidia watoto bila kujali kabila wala dini.

“Mimi binafsi kama mzazi nimefurahi sana kwa sababu kuna watoto wengi walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa pesa, na najua vile gavana ameingilia kati, watasaidika,” alisema Mary.