Mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili uvumi ulienea hewani kuwa Soko la Nyakongo wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazi litajengwa ili kuwa soko la kisasa.
Wafanyi biashara walijawa na furaha wakiwa na matumaini ya kuepukana na hali mbaya ya anga ikiwemo mvua na jua kali ambalo walikuwa wakistahimili kwa miaka na mikaka.
Tangu siku hiyo soko hilo limekuwa chini ya ujenzi hadi sasa. Kulingana na wafanyi biashara ni miaka minne sasa inaelekea kukamilika. Soko hilo linaonekana kukamilika lakini bado limefungwa.
Unapolitazama soko hilo kwa umbali kweli ni la kisasa, lakini je, linasubiri yesu kurudi ili alifungue?
Wakizungumza kwa njia ya simu, wafanyi biashara hao amabao hawakutaka majina yao kutajwa wanaomba serikali ya kaunti ya Kisii kulifungua soko hilo kwa haraka.
“Tunasumbuka kwa jua, mvua na soko tunaliona tu kwa picha kwani nani amejengewa. Tumengoja sasa ni miaka minne inaelekea kuisha na hatuoni chochote ni sinema tu tunaona," walisema wafanyibiashara hao.
"Juzi wameweka taa tunashukuru lakini tunaumia juu ya mvua na jua. Wakati walianza kujenga tulikuwa na matumaini tukaimba na kushukuru lakini sasa hatuoni kinachoendelea," waliongeza wafanyibiashara hao.
Tunamwomba Gavana Ongwae ajue hapa ndio mama yake ananunua mboga amelelewa hapa akija nyumbani nyama ananunua hapa, sukuma anapata hapa, sukari kila kitu anapata hapa kwa hivyo mahali alipo yeye ni mtoto wa hili soko atuangalie na sisi tufurahie kuwa mtoto wetu ametukumbukaka," walilama wafanyibiashara hao.