Mwenyekiti wa wanabiashara katika mji wa Kisii Elijah Ombongi amemwomba gavana wa kaunti ya kisii James Ongwae kukarabati soko mpya aliyofungua hivi karibni katika eneo la St Judes mjini Kisii.
Akiongea siku ya Jumatatu katika uwanja wa Gusii katika sherehe za siku kuu ya Madaraka, mwenyekiti huyo alimwmba gavana Ongwae kukarabati soko hilo kwa kujenga vibanda, ili wanabiashara wasiwe wanasumbuka haswa wakati huu wa mvua nyingi ambayo inaendelea kunyesha katika mji wa Kisii.
“Naomba gavana wetu ujenge vibanda katika soko hii yenye ulifungua maana wanabiashara husumbuka mvua inaponyesha, ukijenga vibanda, wanabiashara watakuwa katika hali nzuri,”alisema Ombongi.
Aidha, mwenyekiti huyo alimtaka Ongwae kuwakumbuka wanabiashara wote wa kaunti ya Kisii wanapoenda kupitisha mswada wa kiwango cha pesa wanabiashara wanastahili kutozwa.
“Wengi wa wanabiashara wako na biashara vidogo ambavyo vinaweza kugharimu shillingi 2,000, na wakitozwa ushuru wa juu, hiyo ni kumaanisha watafunga kufanya biashara zao. Naomba uangalie sana upande wa wanabiashara kiwango cha ushuru watatozwa,” aliongeza Ombongi.
Kwa upande wake, Ongwe alisema kuwa wakati mkutano unapoandaliwa kuzungumzia pesa za ushuru, wengi hawafiki na wanajitokeza kulalamika baadaye.
Ongwae alisusia kujibu swali la kuhusu kujenga vibanda kwa soko hiyo mpya aliyoifungua.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongonzi mbalimbali wakiwemo naibu gavana wa Kisii Joash Maangi, Mbunge wa Nyaribari Chache Richard Tongi na wawakilishi wengine walikuwa kwa sherehe hiyo.