Seneta wa Kaunti ya Nyamira Kennedy Okong'o amempongeza Gavana John Nyagarama kwa hatua aliyochukuwa kuwarejesha maafisa walioondolewa madai ya kujihusisha na ufisadi kazini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza kwenye hafla ya mazishi ya Dkt Joel Momanyi kwenye ukumbi wa shule ya upili ya Nyangoge, siku ya Ijumaa, wiki jana, Okong'o alisema kuwa gavana hakuwa na budi kufanya hivyo baada ya bunge la kaunti hiyo kuitupilia mbali ripoti hiyo miezi michache iliyopita.

"Napongeza Gavana Nyagarama kwa hatua aliyochukua kuwarejesha maafisa hao kazini kwa kuwa kisheria, hakuwa na budi ila kufanya hivyo kwa kuwa tayari bunge la kaunti hiyo lilikuwa limeitupilia mbali ripoti iliyowahusisha baadhi yao na ufisadi," alisema Okong'o.

Aidha, seneta huyo aliwaonya wawakilishi wa wadi dhidi ya yakushawiwa kutupilia mbali ripoti iliyokuwa ikiwahusisha mawaziri hao na makatibu wao na ufisadi.

Alisema kuwa hatua ya wawakilishi wa wadi kuitupilia mbali ripoti ya kamati teule iliyokuwa ikichunguza maafisa hao wa kaunti waliohusishwa na ufisadi huenda ilisababishwa na maafisa husika ili kuficha ukweli.