Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua amewashangaza wengi kwa kula chamcha katika kibanda kimoja katikati mwa soko mjini Nakuru.
Haya yalijiri punde tu baada ya Gavana Mbugua kufungua rasmi bustani iliyokarabatiwa ya Lions mjini Nakuru.
Akiwa ameandamana na mwakilishi wadi ya Bishara Stephen Kuria, mwenzake wa London Francis Njoroge na mwakilishi mteule Rosemary Okemwa, walipata chakula ikiwemo chapati kwa maharagwe katika vibanda vya sokoni.
"Sisi kama viongozi wenu hakuna cha kutuzuia kula hapa, ndiposa tumepitia tujumuike pamoja na hata mjue serikali inajali maslahi yenu kama wafanyibiashara wadogowadogo," alisema Mbugua.
Ni hatua iliyopongezwa na wengi wa wakazi, ambapo walisema ni kuonyesha kiongozi wa watu.
"Kama gavana anaweza kula kwa kibanda, basi ni dhihirisho kwamba anajali hata wananchi wa chini," alisema mmoja wa wakazi.