Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama ametenga milioni 63 kwa ujenzi wa uwanja wa michezo katika eneo la Manga, lililoko eneo bunge la Kitutu Masaba Kaunti ya Nyamira ili kuinua uchumi wa eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea katika uwanja wa michezo wa Manga ambapo alianzisha ujenzi wa uwanja huo, gavana Nyagarama alisema anahitaji kuona eneo hilo likipanda kibiashara na kiuchumi huku akiwaomba watu kulinda mradi huo.

“Hakuna yeyote amewahi leta pesa nyingi katika eneo hili bali mimi, vile nilisoma hapa nimeleta pesa shillingi million 63 kwa ujenzi wa soko, vile niliona soko la eneo hili litaanguka kibiashara ndiposa nikaanzisha mradi huo,” alisema Gavana Nyagarama.

“Mradi ambao nimeleta katika eneo hili utawafaidi vijana wa umri mdogo haswa katika kugundua talanta zao,” aliongezea Nyagarama.

“Nawaomba wazazi wenzangu, watoto wenu sasa wamepata fursa ya kukuza talanta zao na ninawahidi kuwa nitaweka kituo kingine mahala hapa eneo la Manga kama kile tayari tumeanzisha eneo la kiabonyoru ili talanta za watoto kukuzwa,” aliongezea Nyagarama

Wakaazi wa Nyamira walimpongeza gavana wao kwa kuanzisha ujenzi wa uwanja huo, huku wakiwa ma matumaini makubwa kwambu utawasaidia kwa kiasi kikubwa.