Gavana wa Kaunti ya Nyamira John Nyagarama amewahakikishia wananchi wa kaunti hiyo kuwa watapata huduma bora katika sekta ya afya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea siku ya Jumanne katika hospitali ya Motagara iliyoko eneo bunge la Mugirango Magharibi kaunti ya Nyamira, Gavana Nyagarama alisema wananchi wa kaunti hiyo watapata huduma bora katika sekta ya afya kwa kuweka mikakati kabambe ya kununua mashene mabalimba li za kupima magonjwa na kubaini mgonjwa ameathirika na ugonjwa upi mwilini.

Hii ni baada ya mbunge wa eneo bunge la Mugirango Magharibi, James Gesami pia aliyekuwa katika hospitai hiyo ya Motagara kumtaka  gavana huyo kuinua huduma ya ya afya na kununua madawa ya kutosha katika hospitali za kaunti hiyo. 

Gesami alisema sharti wananchi wa kaunti hiyo washughulikiwe kikamilifu na serikali ya kaunti hiyo.

Aidha, hospitali ya Motagara ilikabidhiwa kuwa chini ya uongonzi wa kaunti baada ya kujengwa na mbunge wa eneo hilo kwa pesa za hazina ustawi maeneo bunge.

Mbunge Gesami alikabidhi kaunti ya Nyamira hospitali hiyo na kumwomba Gavana Nyagarama kununua mashene zaidi na madawa ya kutosha ili wananchi kufaidika na matokeo ya ugatuzi waliopigia kura wakati wa kupitishwa kwa katiba mpya.

“Nataka sekta ya afya katika kaunti hii iwe na sura mpya ili wananchi wafurahie matunda ya serikali za kaunti. Nakuomba Gavana Nyagarama kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa njia ya kueleweka,” Gesami.