Akina mama kutoka Kaunti ya Nyamira wameombwa kutumia vizuri mikopo wayaochukua kutoka kwa mashirika ya kifedha ili kujiendeleza.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubu kwenye Wadi ya Bokeira alipotembelea kundi la akina mama siku ya Jumatano Gavana wa Nyamira John Nyagarama alisema kwamba kumekuwa na ripoti za baadhi ya akina mama kukosa kulipa mikopo wanayochukua kutoka kwa mashirika ya kifedha hali inayo athiri pakubwa mashirika hayo.

Nyagarama aliwahimiza akina mama kufanya utafiti kabla yakuanzisha biashara ili wasije wakapata hasara kwa kuanzisha biashara zisizokuwa na faida.

"Unapopata mkopo wako ni jukumu lako kuhakikisha kuwa unatumia pesa hizo vizuri kwa maana hatutaki kusikia kuwa baadhi yenu mumekataa kulipa mikopo hiyo, hali inayoathiri mashirika mengi ya kifedha,”alisema Nyagarama.

Gavana Nyagarama pia aliwahimiza akina mama kujisajili kupokea pesa za maendeleo ya akina mama almaarufu 'Women Enterprise Fund', ili kuanzisha biashara zitakazo wasaidia luimarika kiuchumi.

"Ni jambo lakushangaza kwamba baadhi ya akina mama wangali bado wanategemea waume wao hata baada ya serikali kuu kutenga pesa za wanawake kujiendeleza. Ni wakati wenu kujisajili kupokea mikopo hiyo ili kujiendeleza,” alisema Nyagarama.