Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amewataka wawekezaji kuhakikisha wana vifaa vya kuzima moto.
Akiongea kwenye eneo la viwandani kaunti ya Nakuru, Mbugua amesema wawekezaji wa viwanda vya mafuta na biashara nyinginezo wanafaa wawe na vifaa vya kuzima moto ili kukabiliana na mikasa ya moto kabla ya wazimamoto kufika.
“Ni vyema kujitayarisha ili kukabiliana na moto kabla ya wazimamoto kufika,” alisema Mbugua.
Mbugua alikuwa amezuru kiwanda kimoja Jumatano jioni kilichochomeka baada ya mafuta kushika moto.
Gavana Mbugua alikuwa ameandamana na katibu wa kaunti Joseph Motari pamoja na maafisa wengine wa kaunti.