Jimbo la Nakuru limetajwa kama eneo ambalo limeadhirika pakubwa na mvua nyingi inayoendelea kunyesha nchini.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kaunti hiyo sasa imetenga shillingi millioni 12 zilizokuwa za kukabiliana na mvua ya El Nino ili kushughulikia jangi hili.

Kulingana na gavana Kinuthia Mbugua, barabara nyingi zimeharibika. 

"Mwaka uliopita tulitenga shillingi milioni 12 kukabiliana na El nino, hizo fedha hazikutumika kwa hivyo tutazitumia kukidhi madhara ya mvua hii," alisema Mbugua. 

Aliendelea kusema kazi ya kurekebisha barabara zilizoharibika itaanza. 

Alikua akiongea na wanahabari katika uwanja wa Gilgil kwenye hafla ya siku mbili ya Gavana Mtaana.

Mkuu huyo wa kaunti alisema mradi huu unaleta huduma karibu na wananchi hata wale ambao wako mashinani.